Shehena kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa
kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini imenaswa katika bandari
ya Zanzibar huku ikishuhudiwa na mawaziri wa serikali zote mbili
wakiongozwa na waziri wa mali asili na utalii Mhe Khamis Kagasheki.
Shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea
Philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na magunia
mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini
yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa
kusafirishwa kwenda Philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka
husika za bandarini.
Wakiongea na wandishi wa habari katika bandari ya
Zanzibar waziri wa nchi afisi ya rais utawala bora na idara maalum Mhe
Haji Omar Kheri amesema hii ni janga kubwa la nchi na serikali kamwe
haitokubali kuona wahusika wanaanchiwa na kuahidi sheria kufanya kazi
yake ,kwa upande wake waziri Kagasheki ambaye aliwisili Zanzibar
asubuhii kushuhudia shehena hiyo amesema ni lazima mtandao utokomezwe
kwani utamaliza tembo wa nchii hii na kuipoteza rasilimali ya nchi.
Kwa upande wake kamishna wa jeshi la polisi
Zanzibar CP Mussa Ali Mussa amesema polisi imekamata watu wawili
wazalendo na inaendelea kuwahoji na kufanya upekuzi nje ya bandari
pamoja kwamba taarifa zinaonyesha kuwa mzigo huo ni wa raia wa China.
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment