Thursday, 14 November 2013

Wanandoa wawili huko China wauza watoto wao ili kulipia iPhones na Viatu.

Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha, familia ya wanandoa wawili huko Shanghai imeshitakiwa kwa tuhuma za  kuwauza watoto wao watatu wa kuwazaa wenyewe ili kuweza kumudu gharama za kulipia iPhones, Komputa na viatu vya gharama ya juu.

Mamlaka za nchini China zinaripoti kuwa, Mume na Mke wanaojulikana kwa majina ya Teng na Zhang, wote wakikadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, wanakabiliwa na mashitaka kadhaa ya kusafirisha wanawake na watoto. Mume yupo rumande na mkewe amepata dhamana.

Polisi katika mji wa Shanghai walianza kuchunguza mienendo yawanandoa hao mwezi Mei mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa wanandoa hao walitumia mtandao wa QQ kuweka tangazo la kumuuza binti yao mchanga. Mtandao huo ni maarufu huko China kwa kupelekeana ujumbe mfupi. Polisi waliwapata wanandoa hao baada ya kufuatilia anuani (IP address) ya Komputa yao kupitia tangazo hilo.

Baada ya Polisi kuwakamata, wanandoa hao walikiri kuwauza watoto wao wachanga,watatu , katika kipindi cha miaka ya karibuni kwa jumla ya dola za kimarekani 13,000. 

Walimuuza mtoto wao wa kwanza mwaka 2008, wapili mwaka 2011 na watatu (wa kike) mwaka huu. Mamlaka zimefanikiwa kumpata mtoto huyo wa kike na sasa zinaendelea kuwatafuta wengine wawili.

Majirani wamewaeleza polisi kuwa familia hiyo bado inaishi na watoto wao wengine wawili walio na umri wa miaka 6 na 9. Majirani pia walisema kila mara Mke alionekana mjamzito lakini vichanga havikuonekana muda mfupi tu baada ya kuzaliwa.

Baada ya kufuatilia taarifa za kadi ya benki ya na miamala ya kibenki ya Mke polisi waligundua kuwa wanandoa hao walitumia fedha zao zote za mauzo ya watoto wao kwa kununulia simu aina za iPhones na viatu vya anasa. Pia walinunua komputa kadhaa ambapo polisi walifanikiwa kukuta vitu hivyo vyote nyumbani kwa wanandoa hao.

Wanandoa walidai kuwa waliwauza watoto wao kwa matumaini kuwa watoto hao watapata maisha bora zaidi na pia watu walijitolea kuwapa fedha ingawa wao hawakudai malipo yeyote kutoka kwa watu waliochukua watoto hao.

Hata hivyo taarifa zinadai kuwa suala la kuuza watoto nchini China ni limekuwa ni tatizo kwa miaka kadhaa iliyopita. Mwaka 2011 Wizara ya ulinzi wa uma ilitangaza kusambaratisha mitandao miwili ya kuuza na kusafirisha watoto na kuwaokoa watoto wachanga wapatao 29 katika jimbo la mashariki la Shandong. Watoto hao waliuzwa na wazazi wao wa kuwazaa.

Chanzo: CNN


Aliyemuua mtoto wa miaka mitatu aomba asinyongwe, achangie viungo kwanza.

Hukumu ya kunyongwa kwa Ronald Philllips aliyepatikana na hatia ya kumuua mtoto wa miaka mitatu katika jimbo la Ohio nchini Marekan imeahirishwa kutokana na mshitakiwa huyo kuomba kuchangia baadhi ya viungo vyake vya mwili zikiwemo figo ili kunusuru uhai wa mama anayeumwa.

Ronald Phillips alitarajiwa kunyongwa Alhamis kwa njia ya sindano ya sumu baada ya kupatiakana na hatia ya kumuua mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu mwaka 1993.

Gavana wa jimbo la Ohio John Kasich amesema kama ombi hilo la mshitakiwa litasaidia kuokoa uhai wa mtu mwingine basi na likubalike, lakini litakuwa jambo geni kuahirishwa kwa adhabu iliyokwisha kupitishwa japo kuwa madaktari wanapaswa kuthibitisha.

Phillips mwenye umri wa miaka 40 alihukumiwa kifo kutokana na makosa ya ubakaji na mauaji ya binti wa rafiki yake wa kike Sheila Marie Evans.

Dawa ya sumu iliyotarajiwa kutumika kumuua Phillips ni aina ya midazolam na hydromorphone, mchanganyiko wa dawa ambayo ingetumika kwa mara ya kwanza nchini Marekani kunyonga watu
Jimbo la Ohio liliamua kutumia mchanganyiko wa dawa hii kwa sababu haikuwa na kiasi cha kutosha cha dawa ya kawaida inayotumika kunyongea watu ijulikanayo kama pentobarbital.

Mama mzazi wa Phillips amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo na dada yake Phillips pia anasumbuliwa na maradhi ya moyo ambapo anasema anahitaji kutoa viungo vyake haraka iwezekanavyo. 


Chanzo: BBC

Je umechoshwa na foleni za benki? Tazama ubunifu huu.

Kama umechoshwa kukaa katika misururu mirefu ya benki ukisubiri kuhudumiwa, ubunifu huu hapa katika picha waweza kusaidia. Je njia hii yaweza fanikiwa hapa bongo?


Siku njema!

Wednesday, 13 November 2013

Shehena kubwa ya meno ya tembo imekamatwa katika bandari ya Zanzibar.

Shehena kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915  ambayo haijawahi kukamatwa nchini imenaswa  katika bandari ya Zanzibar huku ikishuhudiwa na mawaziri wa serikali zote mbili wakiongozwa na waziri wa mali asili na utalii Mhe Khamis Kagasheki.

Shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea Philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na magunia mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa kusafirishwa kwenda Philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka husika za bandarini.

Wakiongea na wandishi wa habari katika bandari ya Zanzibar waziri wa nchi afisi ya rais utawala bora na idara maalum Mhe Haji Omar Kheri amesema hii ni janga kubwa la nchi na serikali kamwe haitokubali  kuona wahusika wanaanchiwa na kuahidi sheria kufanya kazi yake ,kwa upande wake waziri Kagasheki ambaye aliwisili Zanzibar asubuhii kushuhudia shehena hiyo amesema ni lazima mtandao utokomezwe kwani utamaliza tembo wa nchii hii na kuipoteza rasilimali ya nchi.

Kwa upande wake kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa  amesema polisi imekamata watu wawili wazalendo na inaendelea kuwahoji na kufanya upekuzi nje ya bandari pamoja kwamba  taarifa zinaonyesha kuwa mzigo huo ni wa raia wa China.
 
 
Chanzo: ITV

Tuesday, 12 November 2013

Ucheshi/Utani: Muhindi anapojaribu kujibu Vitendawili, mafumbo na Methali



Hivi ndivyo ilivyokuwa pale Muhindi alipojaribu kujibu Vitendawili, mafumbo na Methali;-

(1) Mfa maji?.....… tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?……. tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?…mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua?…uliza google.com.
(5) Mbio za utelezini?….chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga?…ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea?…iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika?… mambie dada ta-deki.
(9) Chelewa chelewa?…takosa guo ya sukukuu…..
(10) Kila ndege .....? Hutua Airport
(11) Bandu bandu ....? Menzie Makame....
(12) Mtaka cha Uvunguni ....? Binua tanda yote
(13) Simba mwenda pole.....? Iko gonjwa kama sio gonjwa iko fungwa na Yanga
(14) Barabara ndefu ....? Ongeza mwendo, tachelewa fika
(16) Mla nawe hafi nawe ila .....? Takimbia
(17) Ujanja mwingi....? Hapana mpa kazi taibia yeye
(20) Akumulikae mchana ....? Iko pofu
(21) Mficha maradhi ....? Taenda Loliondo

 Siku njema...

Monday, 11 November 2013

Jamaa atolewa kaburini akiwa hai



Hii imetokea huko Brazili ambapo jamaa mmoja ametolewa kaburini akiwa hai baada ya kuwa amezikwa kwa bahati mbaya akiwa bado mzima. Tukio hili limetokea katika kitongoji cha Ferraz de Vasconcelos mjini Sao Paulo ambapo mpaka sasa jamaa huyo anaendelea kutibiwa hospitalini.

Jamaa huyo aliezikwa akiwa hai alipataa bahati hiyo ya kuokolewa baada ya mwanamke mmoja muombelezaji aliposikia kelele zikitokea ndani ya kaburi.


Inaarifiwa kuwa mwanamke huyo muombolezaji  aliwataarifu polisi juu ya sauti aliyoisikia kutokea ndani ya kaburi lakini hawakumwamini na iliwabidi wamtafute mtunza makaburi ili aweze kuthibitisha habari hizo.

Picha za video zinamuonesha jamaa huyo akitolewa toka kaburini na akiwa amelezwa katika majani huku hajitambui.


Chanzo

Neno la ufunguzi!

Halo waungwana!, karibuni tena katika kijiwe kingine cha kupashana habari na taarifa mbalimbali juu ya maswala mbalimbali yanayotokea katika uso wa dunia kuwahusu walimwengu na ulimwengu wao.

Katika salamu hizi za kukukaribisha sina mengi saana ila nikuambie tu ukae tayari kupokea habari motomoto mchanganyiko kupitia ukurasa huu , habari za kuelimisha na  kuburudisha zikiwemo pia komedi, utani, katuni au vikaragosi n.k.

Karibu sasa usome zaidi!

Stanslaus MAGANGA.
Mhariri mkuu.