Ajabu na Kweli

Wanandoa wawili huko China wauza watoto wao ili kulipia iPhones na Viatu.

Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha, familia ya wanandoa wawili huko Shanghai imeshitakiwa kwa tuhuma za  kuwauza watoto wao watatu wa kuwazaa wenyewe ili kuweza kumudu gharama za kulipia iPhones, Komputa na viatu vya gharama ya juu.

Mamlaka za nchini China zinaripoti kuwa, Mume na Mke wanaojulikana kwa majina ya Teng na Zhang, wote wakikadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, wanakabiliwa na mashitaka kadhaa ya kusafirisha wanawake na watoto. Mume yupo rumande na mkewe amepata dhamana.

Polisi katika mji wa Shanghai walianza kuchunguza mienendo yawanandoa hao mwezi Mei mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa wanandoa hao walitumia mtandao wa QQ kuweka tangazo la kumuuza binti yao mchanga. Mtandao huo ni maarufu huko China kwa kupelekeana ujumbe mfupi. Polisi waliwapata wanandoa hao baada ya kufuatilia anuani (IP address) ya Komputa yao kupitia tangazo hilo.

Baada ya Polisi kuwakamata, wanandoa hao walikiri kuwauza watoto wao wachanga,watatu , katika kipindi cha miaka ya karibuni kwa jumla ya dola za kimarekani 13,000. 

Walimuuza mtoto wao wa kwanza mwaka 2008, wapili mwaka 2011 na watatu (wa kike) mwaka huu. Mamlaka zimefanikiwa kumpata mtoto huyo wa kike na sasa zinaendelea kuwatafuta wengine wawili.

Majirani wamewaeleza polisi kuwa familia hiyo bado inaishi na watoto wao wengine wawili walio na umri wa miaka 6 na 9. Majirani pia walisema kila mara Mke alionekana mjamzito lakini vichanga havikuonekana muda mfupi tu baada ya kuzaliwa.

Baada ya kufuatilia taarifa za kadi ya benki ya na miamala ya kibenki ya Mke polisi waligundua kuwa wanandoa hao walitumia fedha zao zote za mauzo ya watoto wao kwa kununulia simu aina za iPhones na viatu vya anasa. Pia walinunua komputa kadhaa ambapo polisi walifanikiwa kukuta vitu hivyo vyote nyumbani kwa wanandoa hao.

Wanandoa walidai kuwa waliwauza watoto wao kwa matumaini kuwa watoto hao watapata maisha bora zaidi na pia watu walijitolea kuwapa fedha ingawa wao hawakudai malipo yeyote kutoka kwa watu waliochukua watoto hao.

Hata hivyo taarifa zinadai kuwa suala la kuuza watoto nchini China ni limekuwa ni tatizo kwa miaka kadhaa iliyopita. Mwaka 2011 Wizara ya ulinzi wa uma ilitangaza kusambaratisha mitandao miwili ya kuuza na kusafirisha watoto na kuwaokoa watoto wachanga wapatao 29 katika jimbo la mashariki la Shandong. Watoto hao waliuzwa na wazazi wao wa kuwazaa.

Chanzo: CNN

No comments:

Post a Comment